DIAMOND PLATNUMZ AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MENINA ATICK NA WEMA SEPETU
Hatimaye
Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana
na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na Meninah Atick.
Diamond amesema kuwa tetesi hizo zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa.
“Unajua
hizi habari kiukweli zimekuwa zikinihuzunisha sana,” amesema msanii
huyo. “Unajua mie ni mtu mmoja ambaye sipendi kuzunguzia mambo ya
rumors, siju magazeti huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa najuakabisa
siwezi kubishana na media kwa kuwa media ni kubwa, maana najua utaongea
na huyu na yule siku ya siku utagombana na watu. Ndio maana huwa nakaa
kimya,” ameongeza Diamond.Wema
“Kusema
ukweli hili suala limekuwa likiniumiza ‘eti sijui kuna vikao vya harusi
mie nataka kumuoa Meninah’ Kusema ukweli sina mahusiano na Meninah.
Kila mtu anajua mie nina mahisiano Wema. Wema ndo mpenzi wangu, ila
wakati mwingine nakuwa naelewa ile inakuwa ni trick ya kibiashara. Mtu
anajua hata nikimuandika vipi ‘Diamond sijui kafanya nini watu hawawezi
kumchukia! Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kwa watu kuwa
nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti.”
“Unajua
kitendo hicho kinaniudhi naona mtu yupo na mpenzi wake halafu
anamsaliti. Najua hicho ni kitendo ambacho kila mtu hakimpendezi. Kwa
hiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kupitia njia hiyo. Labda
wana wasanii wao, sasa wanaona tukiingia kwa njia hii tutaweza
kumuharibia Diamond.
Ndio
siku zote nimekuwa kimya tu ila sina mahusiano na Meninah. Mie nikiwa
na mtu huwa sifichi naweka wazi kabisa. Hata kama leo nimeachana na Wema
nasema tu, why nifiche? Mie katika mambo yangu huwa simuogopi mtu kama
ningekuwa nataka kuoa basi ningeweka wazi why nifiche?
0 comments: