HATIMAYE CHIDI BENZI APATA DHAMANA
Chid Benz akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
HATIMAYE msanii wa
muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro 'Chid Benz' leo asubuhi amepata dhamana
baada ya kutimiza masharti ya kesi yake ya kukamatwa na dawa za kulevya.
Msanii huyo, jana alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka matatu ya
kukutwa
na madawa ya kulevya ambapo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana ya
shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili wasiokuwana hatia.
0 comments: