UNAFAHAMU NAMNA WATU HAWA WALIVYOPONA EBOLA? SOMA HAPA



Ebola Survivors
Taarifa kuhusiana na Ebola zimekuwa zikichukua headlines kila siku katika vyombo mbali mbali vya habari duniani, tangu uliporipotiwa kulipuka huko Afrika Magharibi.
Mlipuko wa Ebola umeelezewa kusababisha vifo na maambukizi kwa watu wengi zaidi, kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, ambapo vifo zaidi ya 4000 vikiripotiwa katika nchi za Afrika Magharibi, na wagonjwa zaidi ya 9000 wakiugua kutokana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.
Hakuna tiba ya ugonjwa huo ambayo tayari imethibitika, lakini wapo watu ambao wamewahi kutajwa kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo na wakapona.
CNN kupitia ukurasa wake mtandaoni wameandika majina ya Dk. Kent Brantly, Nancy Writebol, na Dk. Rick Sacra kuwa ni baadhi ya watu waliopata maambukizi ya Ebola wakiwa Liberia, na wakapona.
Maswali ni mengi kuhusiana na watu hao; wamewezaje kupona huku wengine maelfu wakiendelea kupoteza maisha?
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu hao whttp://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/10/Ebola-Survivors.jpgaliosalimika walibahatika kuwashishwa katika hospitali mbili kati ya chache ambazo ziliandaliwa rasmi kwa ajili ya kutoa tiba za magonjwa ya kuambukizwa, kama ilivyo kwa Ebola.
Hospitali ya chuo cha Emory iliyopo Atlanta, pamoja na Nebraska Medical Center zinatajwa kuwa hospitali zilizowatibu wagonjwa hao.
Thomas Duncan aliyefariki siku chache baada ya kugundulika kuwa na maambukizi akitokea nchini Liberia, hakwenda kupata huduma za matibabu kutoka katika hospitali hizo.
Njia nyingine ambayo imetajwa kusaidia baadhi ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa huo ni ile ya kuongezewa plazma katika damu, ambapo mtu ambaye hana maambukizi anaweza kumwongezea plazma mgonjwa aliyeathirika na hivyo kusaidia kumuongezea kinga za mwilini.
Mbali na njia hizo, njia nyingine ambazo zimebainishwa ni pamoja na ile ya mgonjwa kuongezewa maji kwa wingi mwilini na pia wapo ambao walipona kwa dawa mbali mbali ambazo ziko katika majaribio, japo imeelezwa kuwa matumizi ya dawa hizo ambazo hazijathibitishwa ni hatari.

0 comments:

Copyright © 2013. MAPYATZBLOG - All Rights Reserved
Customized by: MAPYATZBLOG | Powered by: http://bongoswagzs.blogspot.com/
Designed by: http://bongoswagzs.blogspot.com//