WANAFUNZI WANAONGOZA KWA KUTAZAMA PICHA NA VIDEO ZA NGONO KWENYE SIMU ZA MIKONONI
BARAZA la Ushauri la Watumiaji Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Iringa (TCRA-CCC) limewahadharisha vijana na matumizi yasiofaa ya huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia simu za mkononi.
“Picha
za ngono na utafutaji wa wapenzi wapya ni sehemu ya huduma katika simu
za mkononi zinazowavutia vijana wengi wakiwemo wanafunzi wa shule za
msingi, sekondari na vyuo,” alisema Mwenyekiti wa baraza hilo, Raphael Mtitu.
Mtitu
alisema kwa kupitia huduma za Whatsapp na Facebook, wanafunzi wamekuwa
wakikutana na marafiki wapya wanaowataka kimapenzi lakini pia wamekuwa
wakibadilishana picha mbalimbali za ngono zinazokinzana na maadili ya
Mtanzania.
“Kuna
picha za video za ajabu zinatumwa kupitia mitandao hiyo. Picha hizo
ambazo kiukweli hazifai kutazamwa na vijana wetu zimekuwa kivutio chao
kikubwa,” alisema.
Alisema
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapaswa kulitazama hilo na
kulifanyia kazi ili kunusuru kundi kubwa la vijana linalobomoka
kimaadili kutokana na matumizi ya huduma hizo katika simu za mkononi.
Naye
Katibu wa Baraza, Edina Byemerwa alisema baadhi ya sinema zinazoigizwa
na Watanzania nazo zinachangia kumomonyoa maadili ya Mtanzania.
“Ni
sinema zinazooneshwa bila kipingamizi chochote, na ndizo zinazoelekea
kupendwa zaidi na vijana wetu tu kwa sababu zinazungumza mapenzi zaidi.
“Nyingi
ni za mapenzi, zinahusu vijana wa kike na kiume kutafutana kimapenzi;
hatujui vijana wetu wanazipendea nini lakini kwa vyovyote yapo
wanayojifunza na hayo yanaweza kuwa ya hatari katika maisha yao,” alisema.
Byemerwa
alisema TCRA haijatimiza wajibu wake katika kusimamia Sekta ya
Utangazaji na ndio sababu yapo mengi yanafanyika kinyume na sheria.
Bila
kutoa mifano ya filamu hizo, Byemerwa alisema kama TCRA itaendelea
kuzifumbia macho zitaendelea kuharibu rika la vijana wengi.
0 comments: