MWANAMKE AHUKUMIWA ADHABU YA KIFO BAADA YA KUMTUKANA MTUME MUHAMMAD.

Mwanamke mmoja amehukumiwa adhabu ya kifo nchini Pakistan kwa kosa la kufuru, naye amekwisha kukata rufaa katika mahakama kuu nchini humo, hukumu hii imekuja miaka minne nyuma baada ya kukutwa na hatia kwa kumtukana mtume Muhammad Swalalahu ale wa Salaam.

Wakiili wa Asia Bibi anaamini kwamba rufaa yao itafanikiwa na mashauri yatakuwa baada ya mwaka mmoja.

Asia anashutumiwa kwa kufuru na kikundi kimoja cha wanawake wa kiislam kwa madai ya bibi huyo kutokuwa tayari kugusa birika la maji baada ya wanawake hao kulishika kwa madai ya imani yake.
 
Bi Asia akiwa na familia yake.
 
Pakistani katika sheria zake haina kawaida ya kunyonga raia wake kwa kosa la kufuru lakini mashtaka, adhabu na vifungo vimekuwepo mara kwa mara kwa makosa ya kuutusi uislam.BBC

0 comments:

Copyright © 2013. MAPYATZBLOG - All Rights Reserved
Customized by: MAPYATZBLOG | Powered by: http://bongoswagzs.blogspot.com/
Designed by: http://bongoswagzs.blogspot.com//