AIBU FUNGA MWAKA! MREMBO WA BONGO MOVIE ANASWA USIKU MNENE
Tukio hilo la kinyaa lilitokea hivi karibuni maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, karibu kabisa na maegesho ya magari yanayotumiwa na ukumbi wa burudani wa New Maisha.Chanzo makini kilichomuona msanii huyo, kilimtonya paparazi wetu siku hiyo baada ya kubaini msanii huyo amekuwa na kamchezo hako kachafu kila anapokwenda klabu hapo.
“Huyu jamaa amekuwa na haka kamchezo ka kwenda kumalizia kwenye parking za magari sasa leo kaja na kabinti f’lani hivi, njooni mmnase,” kilisema chanzo hicho.Bila kupoteza muda, paparazi wetu alitumia usafiri wa bodaboda ndani ya dakika sifuri alifika eneo la tukio ambapo siku hiyo kwenye ukumbi wa New Maisha Club kulikuwa kuna shoo ya Bunyerobunyero iliyokuwa na watu wachache.
Paparazi wetu alimkuta Stan akiwa nje ya gari aina ya Toyota Altezza akivutana kimahaba na mrembo huyo huku wakibusiana na muda mfupi baadaye walizama ndani ya gari hilo ndipo paparazi wetu alipoitendea haki kamera yake kwa kufotoa picha kadhaa.
Stan na mrembo huyo baada ya kushtuka na kuona mwanga wa kamera ukiwawakia kama taa za gari, walikurupuka na kuanza kumpiga mkwara paparazi wetu ambaye alisimamia kazi yake kikamilifu ndipo mrembo huyo aliyekuwa ametinga kigauni kifupi cheusi alipotimua mbio baadaye Stan naye akamfuata na kutokomea.
0 comments: