BABY MADAHA MAPENZI NI HOBI YANGU


Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha.
Stori: Gladness Mallya
MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Baby Madaha alisema ‘hobi’ yake ni mapenzi japokuwa anapenda muziki lakini haifikii jinsi anavyoyapenda mapenzi kwani yanampumzisha akili yake na kumfurahisha moyo wake pia.
“Ukweli napenda mapenzi kuliko kitu chochote ila sipendi kuzinguliwa na wanaume, ninapenda muziki, filamu lakini haviwezi kufikia mapenzi kwani ndiyo kila kitu kwangu na yananipa starehe kuliko kitu chochote hapa duniani,” alisema Baby Madaha.

0 comments:

Copyright © 2013. MAPYATZBLOG - All Rights Reserved
Customized by: MAPYATZBLOG | Powered by: http://bongoswagzs.blogspot.com/
Designed by: http://bongoswagzs.blogspot.com//