BREAKING NEWS: ASKOFU MWANAMKE ACHAGULIWA UINGEREZA

Kanisa la Uingereza limemchagua askofu wa kwanza mwanamke.Mchungaji
Libby Lane atakuwa askofu wa Stockport mnamo mwezi January ,na kumaliza
ukiritimba wa wanaume kuwa maaskofu katika kanisa hilo.Amesema kuwa
amefurahishwa na hatua hiyo.Kanisa la Uingereza liliwachagua wanawake
mara ya kwanza kama makuhani mnamo mwaka 1994.Wanawake tayari
wameruhusiwa kuwa maaskofu katika maeneo mengine ya jamii ya kianglikana
,ikiwemo Marekani na kusini mwa Afrika.
CHANZO: BBC SWAHILI
0 comments: