BREAKING NEWS: WABUNGE KENYA WATWANGANA BUNGENI..WATOANA VIDONDA !

Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku
wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama
ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.


Bunge la Kenya
Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu
kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge
walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo
wakisema 'bado mapambano.'
Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge
kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao
ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa
usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw
augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya
uchunguzi.

Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari
yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au
picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa
Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia
Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa
tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya
kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
CHANZO: BBC
CHANZO: BBC
0 comments: