HII NDIO ONYOOO...Rose Ndauka Awapasha Wanaofuatilia Maisha Yake...Kisa Namkasa? Picha Hizi!!
Mrembo na mwigizaji wa filamu za hapa bongo,
Rose Ndauka ambae ni mama wa mtoto mmoja amewatolea uvivu baadhi ya watu
ambao ni “followers” wake kwenye mtandao wa Instagram ambao
walimshambulia sana kwa maneno baada ya yeye kuweka picha hiyo hapo juu
akiwa amekaa na “jamaa” huku amemfunika uso.
Chokochoko
Baadhi ya watu hao walichukulia kwamba huyu
jamaa pichani ndio “PROJECT” mpya ya Rose hivyo wakaanza kumshabulia
mwananadada Rose kwa maneno kuwa hajatulia na ndiomana aliachika kwa
bwana, na wengine wakisema kwa yeye kwasasa anamtoto mdogo kwa hiyo
inampasa atulie na amlee mtoto kwanza na sio kufanya maswala kama
hayo... na mengine mengi tu. Huku “followes” wake wengi wakionekana
kumuunga mkono Rose kwa alichoonekana kukifanya kwani ana haki ya
kufanya kile roho yake inapenda, hivyo basi ni vyema watu wamuache na
waache “PROJECT” iendelee.
Rose Awashukia
Baada ya figisufigisu yote hiyo hatimaye Rose mwenye alifunguka kama ifuatavyo;
“instfamily love them so much#ushauri mdogo
kwa wale wanaopenda kuwapangia watu namna ya kuishi,tafutene ofisi ili
tuweze kuja na kuwaeleza ili mkiwa mnatupangia uwe unajua vizuri kuhusu
mtu husika sio kukurupuka tu,acheni ushamba duh mnanichosha kwakweli.Tag
mtu yeyote mwenye tabia ya kukurupuka na kuongea asichokijua loooh”
Nadhani ujumbe umefika.Sina neno lakuongeza hapo
0 comments: