HUNDI YA WAPONZA MISS TANZANIA
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema moja ya sababu ya
kufungia mashindano hayo ni waandaaji, Kampuni ya LINO kutoa hundi feki
ya malipo ya kibali ya Sh2Milioni.
BARAZA la
Sanaa na Taifa (Basata) jana Jumatatu lilitoa sababu za kuyafungia
mashindano ya Miss Tanzania kwa miaka miwili ikiwemo Kampuni ya LINO
kuwasilisha hundi feki katika baraza hilo.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema moja ya sababu ya
kufungia mashindano hayo ni waandaaji, Kampuni ya LINO kutoa hundi feki
ya malipo ya kibali ya Sh2Milioni.
“Walituletea
hundi muda mfupi kuelekea siku ya shindano tukawaamini lakini kumbe
ilikuwa feki na hadi leo leo hawajalipa,” alisema.
Mkurugenzi
wa LINO, Hashimu Lundenga alisema: “Basata walichelewa kuipeleka benki
hundi tuliyowapa, lakini tunakiri ilikuwa na makosa na tumekubaliana
tutawalipa.
”CREDIT
: MWANASPOTI
0 comments: