KILICHOTOKEA JANA KUHUSIANA NA HABARI ZILIZO IHUSU BENKI YA NBC
Nianze
kuliandikia hili kwa kuonyesha furaha yangu kuwa huwenda sasa kumekua na uelewa
juu ya maswala ya usalama mitandao. Nalisema hili kutokana na uhalisia kwamba
Jana nilipata maswali kutoka kwa watu wengi sana huku nikipata jumbe nyingi
zilizofanana zikielezea juu ya tukio la benk ya NBC kuingiliwa na wadukuzi.
Wengi
walinitaka pia nielezee huku nikiulizwa mbona hakuna nilichozungumza.
Nilifarijika sana kwani muda uliopita wengi hawakua wakihoji juu ya maswala ya
udukuzi pamoja na usalama mitandao na huwenda hii ilitokana na kutokua na
uelewa wa maswala husika.
NINI HASA KILITOKEA?
Kwanza
kabisa Kulikua na Itlafu ya Umeme ambayo ilisababisha baadhi ya Mashine kuzima.
Pili,
Kulitokea Tahadhari ya Moto iliyosababisha wafanyakazi kuchuukua tahadhari ya
kutoka nje.
Na Tatu,
Mifumo ya Mobile banking (Inayotoa huduma za miamala kupitia simu za kiganjani)
kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo iliyo sababisha kutoa kiwango kisicho sawa
kwa waliokua wakiangalia salio.
Matukio
haya matatu yaliunganishwa na kutengeneza taarifa moja iliyo sambazwa kua kuna
mdukuzi aliingilia banki ya NBC na kusababisha mifumo kutofanya kazi na hatimae
kuhamisha kiasi kikubwa cha pesa. Kitu
ambapo kilipelekea wafanya kazi kutoka nje ili uchunguzi zaidi uweze kufanywa.
Na
anaepata taarifa anapo angalia salio anaona kunatatizo katika kiasi chake na
kuamini jumbe ile. Panapotoka ufafanuzi wa taarifa hii wengi bado wanahoji bado
kuna shaka niendelee kutoa ufafanuzi nini hasa kinaweza kikawa kimesababisha?
NINI KINAWEZA KUWA TATIZO?
Wengi
wanaweza kuhusisha matukio mawili ya mifumo kuzimika na mifumo ya Mobile money
kutofanya kazi (Kuzidiwa nguvu) na kutoa taarifa zisizo sahihi na kinacho
julikana kama "DDOS ATTACKS" ambapo pia ni uhalifu mtandao unaoweza kusababisha
tukio la mifumo kuzima na kuzidiwa kufanya kazi.
Lakini
pia ikumbukwe mifumo kuzima na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi huwenda
ni maswala tu ya kiufundi na isi husiane kabisa na uhalifu nilio uzungumzia.
Panapo
zimika kwa mitambo ya umeme wakati mwingine husababisha komputa kuzima ghafla
kama mifumo ya kuhifadhia moto kutokua vizuri.
Watu
wengi wanapotuma maombbi kwenye mfumo wanaweza kuisababishia kushindwa kufanya
kazi yake ipasavyo kutokana na kuzidiwa nguvu – Hii inafanana na aina ya
uhalifu nilio uzungumzia ingawa huwenda ikawa ni wengi wametaka kwa nia njema
kujua kiasi cha pesa zao baada ya kusikia kuna tatizo.
Niendelee
kuwasihi wa Tanzania, wanapo ona tatizo ni vizuri kulifatilia na kulichunguza
kwa makini kabla ya kulitolea taarifa na pia kuwapongeza kwa dhati kwa kuweza
kuchanganua mambo hadi kuweza kufikiria juu ya uhalifu mtandao ambapo ni hatua nzuri ya uelewa wa maswala ya usalama mitandao
nchini.
Aidha, Nimefahamishwa kua tayari taarifa kuhusiana na tukio hilo lilio ambatana na taarifa zilizo sambazwa limetolewa ufafanuzi na uongozi wa benki hiyo kwa wateja wake. Na Pia Nitafurahi sana kuona pakiwa na wa Tanzania wakiendelea kutaka kujuua zaidi kuhusiana na maswala ya usalama mitandao.
0 comments: