MASTAA WAKUBWA KIBAO WAMPIGIA SALUTI DIAMOND PLATINUMZ!
BAADA
ya Jumamosi iliyopita msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kunyakua tuzo tatu kwenye tuzo za Channel O zijulikanazo kama
Channel O Africa Music Video Awards 2014 (CHOAMVA), zilizofanyika Afrika
Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita, mastaa mbalimbali nje na ndani ya
nchi wamempigia saluti.
Diamond ambaye ameweka rekodi nchini kwa kuwa msanii pekee kuchukua
tuzo tatu kwa mpigo huku tuzo hizo zikiwa ni pamoja na ya Mwanamuziki
Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Video Bora ya Muziki wa Afro Pop,
Mwanamuziki Bora Anayechipukia hivyo alikosa tuzo moja tu ya Video Bora
kwa mwaka.
Msanii
mkali kutoka Nigeria Davido aliyetoa pongezi kwa ‘Diamond Platnumz’.
Katika makala haya tunakuletea baadhi ya mastaa waliompigia saluti
Diamond na kumpongeza kwa hatua aliyofikia.SUNDAY MANGU ‘LINEX’“Ukweli
nampongeza sana Diamond na kikubwa nasema ametisha sana na ametutoa
kimasomaso.”
DAVIDO
“Tanzania imesimama! Diamond Platnumz ameweza tena!” aliandika mwanamuziki huyu wa Nigeria kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
0 comments: