MHESHIMIWA SUGU LAWAMANI KWA KUMTUPA MWANAYE! EX WAKE AFUNNGUKA MAZITO!
Aliyekuwa
mpenzi wake na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, Faiza
Ally amemtupia mzazi mwenzake kuwa hamjali mwanae baada ya kuachana.
Faiza alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV ambapo alikiri kuwa kuachana na Sugu kunaendelea kumuumiza.
“Imeniathiri sana hata hailezeki,” alisema. “Naona hata nikieleza
siwezi kumaliza. Imeniathiri kiasi kikubwa sana, kwa sababu na mwaka
mzima kama nikipumzika kulia ni siku moja.”“Yaani inauma sana mtu ambaye
ulikuwa unamuona wakati wote unaomtaka, ukimpigia simu saa yoyote hata
kama akiwa kazini, akiwa bungeni labda lazima akiona simu yako hata
akiwa hawezi kupokea lazima aku-text kwamba nitakupigia nipo kwenye
situation hii. Lakini inafika wakati nikimpigia hapokei na hata
ukimtumia meseji anakujibu baada ya siku kadhaa. Kwahiyo mimi imefika
wakati nimeona kwamba hajali kwa sababu haiwezekani ukae miezi miwili
mitatu hujamuona mtoto na usimpigie simu hata kusikia sauti yake,”
aliongeza.
“Mwanzo
nilikuwa nasema ndo kwakuwa tumeachana labda hataki kunisikia
itamuumiza lakini sasa hivi ni mwaka. Sasa nimeona sio mtu mwenye
kujali, kwa sababu kama unajali sidhani kama unaweza kukaa mwezi bila
kusikia sauti ya mtoto wako au hujaulizia anaendeleaje. Basi ikafika
wakati nikaona ngoja nibadilishe kila kitu kwaHiyo nikawa nimEblock
Facebook, nikawa nimemblock WhatsApp nikawa nimesema na Sasha ngoja
nimwandike jina jingine yaani ni katika kujisahaulisha tu huyo mtu
hayupo katika maisha yake.”
0 comments: