SAIKOLOJIA YA WANAWAKE KUCHAGUA MWENZA (MCHUMBA) INACHEKESHA SANA, SOMA ZAIDI HAPA
Wanasaikolojia
wakiongozwa na mwanasaikolojia Benedict Jones wamegundua kwamba,
mwanamke akitaka kupima uzuri wa mwanaume ambaye angependa kuwa rafiki
au mpenzi wake, hupenda kujua kama hata wanawake wenzie wanampenda kama
yeye anavyompenda……..
Anavyozidi
kuwaona wanawake wenzie wakitabasamu au kumchekea mwanaume huyo
anapopita mbele yao ndivyo atakavyojua kwamba, huyo mwanaume ni mzuri.
Hali
hii inafahamika kama copycat reflex na ni matokeo ya nadharia ya Darwin
ya mambo ya mabadiliko ya maumbile ya viumbe, kwa mujibu wa wataalamu
hao, yaweza kutumika pale ambapo mwanamke anakumbana na wanaume wengi
wanaomtaka lakini anapata matatizo ya kumchagua yupi na kumwacha yupi.
Au
akiona uchaguzi wa mwanaume bora utamchukulia muda wake mwingi na nguvu
zake hujirahisishia kwa kuchukua uamuzi wa kuwaangalia wanawake wenzie
wanavyomwona mchumba wake mtarajiwa.
Uchunguzi
huu hufanyika bila wanawake wenzie kujua kwa hiyo mwanaume anayeonekana
kuchangamkiwa sana na wanawake wenzake kwa lengo la kumvuta ili awe
mpenzi wake ndiye ambaye atapata uwezekano mkubwa wa kukubaliwa na
mwanamke huyo.
0 comments: