SARATANI YA MATITI NA NAMNA YA KUJICHUNGUZA MWENYEWE
Saratani
ya matiti ni ugonjwa ambao huwapata wanawake na unatokana na athari za chembe
ndogo ama seli kwenye matiti na matokeo yake ni kwamba hubadili mfumo wa
kawaida wa kukua na kuongezeka.
Mabadiliko
haya huanza polepole na yanaweza yakachukua muda mrefu hadi mtu kuweza kujua
kama ana matatizo hayo. Ikiwa katika hatua hizo za mwanzo kwa kawaida huwa
haina maumivu jambo hilo ni moja ya mambo ambayo huchangia baadhi ya wagonjwa
kubaini tatizo hilo wakati tayari limekomaa.
Ni
kutokana na sababu hizo, wanawake hutakiwa kuchunguza afya zao mara kwa mara
kwa sababu ugonjwa huweza kutibiwa kirahisi iwapo utabainika mapema, miongoni
kwa dalili mwa dalili za saratani ya mititi ni uvimbe kwenye matiti ama makwapa.
Titi kubadilika kiumbo, titi kutoa majimaji yakiyochanganyika na damu ama
chuchu kuingia ndani.
Dalili zingine ni rangi ya ngozi ya titi
kubadilika na kuonekana kama ngozi ya nje ya chungwa na ile hali yake ya
kuonekana kuwa na ngozi laini hutoweka.
Mwanamke
anaweza kujinguza mwenyewe maradhi haya ya saratani na kujua kama ameathirika
ama la, kabla ya kufanya uchunguzi huu unapaswa kufahamu masharti yafuatayo:
Kama
anayejichunguza ana umri zaidi ya miaka 20, anapaswa kuhakikisha anaufanya
katika siku ya tano, sita na saba baada ya kumaliza hedhi. Unapaswa kufuata
hatua kwa hatua katika uchunguzi huo. Hizi ni hatua zifuatavyo:
Utakiwa
kuwa na kioo kikubwa kiasi ambachoo waweza kujiona vyema angalau kifua chote.
Tafuta sehemu ambayo mwanga utakuwa unakupiga kifuani na kioo kuwa mbele yake.
Hii
mara nyingi inapaswa kufanywa chumbani ambako mtu aweza kupata faragha kwa kuwa
itampasa kuvua nguo angalu kifua kukiacha wazi. Kioo hicho waweza ukawa
umekitundika ukutani ama sehemu yoyote ambayo utajiona vema ukiwa umesimama.
Vua
nguo na kuhakikisha kifua na tumbo lipo wazi. Hatua ya kwanza jiangalie kwenye
kioo ukiwa umesimama wima na umeweka mikono kiunoni. Angalia kama kuna
mabadiliko katika umbo au rangi ya ngozi ya matiti na kama chuchu zinaonekana
kutumbukia ndani ya titi.
Unaweza
kulinganisha rangi kwa matiti yote mawili na kuona kama zinafanana. Kama
yanatofautiana yawezekana kuna athari, pia kama moja ya titi litaonekana chuchu
imeingia ndani, pia ni moja ya viashiria vya athari ya aina hii ya saratani.
Hatua
ya pili, nyanyua mkono juu na viganja vishikane juu ya kichwa chako. Hapa
chunguza kama kuna mabadiliko yoyote katika mlingano wa ukubwa wa matiti. Kama
moja litaonekana kuwa kubwa zaidi ya jingine pia ni moja ya viashiria vya
athari.
Hatua
ya tatu, hii haihitaji kioo, unachotakiwa kufanya ni kusimama wima na kunyanyua
mkono wa kushoto juu huku vidole vya mkoo wako wa kulia vikiwa vinabinya na
kuachia kwa mzunguko kwenye titi kuangalia kama ndani kuna uvimbe.
Baada
ya kumaliza kwa titi la kushoto vivyo hivyo utafanya kwa titi la kulia. Njia
hii pia waweza kuifanya ukiwa umelala chali.
Hatua
ya nne, ni ya kuchunguza matiti kwa kukamua na kuangalia kama kuna ute
uliochanganyika na damu. Iwapo utakuwepo wa namna hiyo basin i kiashirio kwamba
kuna uwezekano wa kuwa na athari za ugonjwa huu.
Yawezekana
ukawa na uvimbe ama kitu kingine chochote lakini ikawa ni matatizo mengine
yasiyohusu saratani. Wataalamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti ndio
watakaothibitisha kama una atahri hizo na si vinginevyo.
Wataalam
waliofanya utafiti juu ya saratani ya matiti walibaini kwamba hali hiyo inaweza
kusababishwa na sababu mbalimbali.
Sababu
hizo ni kama vile kuanza hedhi katika umri mdogo, kukoma hedhi katika umri
mkubwa, mwanamke kufikisha umri bila kuzaa na utumiaji wa mafuta mengi katika
mlo.
Mambo
mengine yanaweza kuchangia saratani ya matiti ni mama kutonyonyesha baada ya
kujifungua ana kumnyonyesha kwa muda mfupi. Kuna kina mama wenye tabia ya
kutaka, kutonyonyesha kutokana na sababu zao mbalimbali ambazo mara nyingi siyo
za msingi.
Mambo
mengine ambayo yanachangia mtu kupata saratani ya titi ni unene kupata kiasi,
kutofanya mazoezi mara kwa mara, uvutaji wa sigara, matumizi ya pombe kupita
kiasi, wa wakati mwingine inaweza kurithiwa kutokana na historia ya saratani ya
matiti katika jamii husika.
Mgonjwa
wa saratani ya matiti aweza kupata tiba na kupona kabisa hivyo hakuna haja ya
kuwa na wasi wasi. Hata hivyo, kama nilivyoeleza awali, mtu anapaswa kuibaini
mapema kwa sababu ni wakati ambao anaweza akapatiwa tiba na kupona kwa urahisi.
Aina
zote za saratani ni kwamba zinapaswa kuibainiwa mapema kwa kuwa hiyo ndiyo njia
pekee ya kuweza kuitibu na kupona bila ya mtu kupata matatizo mengi. Zipo aina mbalimbali za tiba na mojawapo ni
upasuaji. Upasuaji huu kwa kawaida hufanywa katika hatua za mwanzo.
Njia
nyingine ni tiba ya mionzi au kupewa dawa. Jambo la kukumbukwa ni kwamba
ugonjwa huu unaweza kusababisha kifo iwapo hautabainika mapema na kupatiwa tiba
mwafaka.
Njia
ambayo mtu aweza kujilinda asiathirike na saratani hii ya matiti ni
kujichunguza mara kwa mara ili kubaini mapema ma kupatiwa dawa.
Kwa
kawaida ,mwanamke anapaswa kuchunguzwa mara moja kwa mwaka ili kuona kama
ameathirika na ugonjwa huo au la.
0 comments: