WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII
WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII
Habari za wiki hii mpenzi msomaji. Mimi
namshukuru Mungu kwa kuweza kunikutanisha na nyinyi kupitia safu hii
ambayo pamoja na mambo mengine nazungumzia juu ya mada mbalimbali ambazo
zinagusa maisha yetu ya kila siku.
Wiki hii nitazungumazia juu ya aina ya
wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa. Wanaume wengi wanapofikia
hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye
sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya
wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha
maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba
kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza
muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba
kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na
kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una
asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba
zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi
ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira
mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia
kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata
mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata
watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake
wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa
na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba
yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio
kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na
mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako
kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha
mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha
mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye
mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo?
Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama
waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku
utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru
mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari
kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa
kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya
ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi
sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke
ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza
kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.
WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na
tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida.
Lakini linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana
kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana
wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa
wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya. Naweza
kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa
wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao
nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia
kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo
yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo
imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo
mwanamke.
WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya
aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke
ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na
uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo
kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale
ambao wako mijijini na hata vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni
mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi
amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda
wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha
yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri
kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.
WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za
ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake
ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake
naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi
dear?" Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia
akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye
Pub anakuambia, "mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena
Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na
usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika mazingira
magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika
maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha
itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa
kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema,
‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’
hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu
kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale
ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa
haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia
ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa
mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa,
yeye anasubiri leo amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho
akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe
wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una
shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza
kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho
unakihitaji upo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na
kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha
ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo.
WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa
katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza
kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona
uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu
na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume,
huyo siyo mwanamke wa kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi
inapotea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa
namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu
atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke
mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari
kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa
ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana
tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao
wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka
jamii.Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika,
wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya
wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo
mbalimbali jijini Dar-es-Salaam. Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto
kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina
gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na
kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya
tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.
0 comments: