FLORA: AFUNGUKA JUU YA UJAUZITO WAKE... ASEMA KUZAA NI RAHA


Msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi ‘H-Mama’ amewashinikiza wasanii wenzake wa kike kuzaa mapema huku akiwataka kuingia kwenye hatua ya kuitwa mama na kusema kuzaa kuna raha yake. 

Akizungumza na paparazi huru, Flora alisema baadhi ya mastaa wamekuwa na dhana potofu kwamba, ukizaa unazeeka na utakuwa hufanyi starehe, jambo ambalo halina ukweli. 

“Mimi nawashauri wazae tu, kuzaa kuna raha yake bwana. Unajua starehe haziishi, kikubwa ni wao kuzaa fasta kisha mambo mengine yanaendelea huku tayari wakiwa wameshaweka ile heshima ya kuitwa mama,” alisema Flora.

0 comments:

Copyright © 2013. MAPYATZBLOG - All Rights Reserved
Customized by: MAPYATZBLOG | Powered by: http://bongoswagzs.blogspot.com/
Designed by: http://bongoswagzs.blogspot.com//