Msichana wa miaka kumi ajilipua Nigeria... ISOME HII HAPAA

Mlipuaji wa kujitolea muhanga ajilipua katika soko moja Nigeria
Mlipuaji wa kujitolea muhanga amejilipua katika soko moja katika mji wa kazkazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa mlipuaji huyo ni msichana wa miaka kumi.
Duru kutoka hospitali zimeambia BBC kwamba takriban watu 15 wameuawa.
Hakuna mtu aliyekiri kutekeleza shambulizi hilo kufikia sasa.
Hatahivyo watu wanalishuku kundi la Boko Haram kutokana na misururu yake ya mashambulizi katika mji huo na maeneo mengine ya Nigeria Kazkazini.
Takriban watu elfu ishirini wamelazimika kutoroka na inahofiwa kuwa mamia waliuawa wakati Boko Haram lilipochukua udhibiti wa mji wa Baga na viungani mwake wiki iliopita.
 Chanza: bbc



0 comments:

Copyright © 2013. MAPYATZBLOG - All Rights Reserved
Customized by: MAPYATZBLOG | Powered by: http://bongoswagzs.blogspot.com/
Designed by: http://bongoswagzs.blogspot.com//