AIBU DAR: DANGURO LINGINE HATARI LAFUMULIWA SHULENI SINZA, MKE WA MTU ANASWA LIVE AKINGONOKA NA NJEMBA. SHUHUDIA MWENYEWE HAPA!
Kikosi cha OFM kikimkurupusha mke wa mtu aliyekuwa akifanya uzinzi na njemba moja(jina halikufamika).
Tukio hilo la aibu ya karne lilijiri ndani ya eneo la shule ya msingi
Shekilango, iliyopo Mapambano, Sinza jijini Dar, hivi karibuni ambapo
mke huyo wa mtu alikuwa akichepuka.
Awali, OFM ilipokea taarifa za kuwepo kwa uchafu huo kutoka kwa
wasamaria wema wanaoishi eneo hilo baada ya kukerwa na tabia hiyo chafu
huku wakiacha kondom zikiwa zimezagaa na kuhatarisha afya za watoto wao
ambao huchezea mipira hiyo ya kinga kama mapulizo.
Baada ya OFM kunyetishiwa ishu hiyo, walishirikiana na askari hao ambapo walivamia eneo hilo na kumbamba mwanamke huyo akibanjuka na njemba.
Baada ya OFM kunyetishiwa ishu hiyo, walishirikiana na askari hao ambapo walivamia eneo hilo na kumbamba mwanamke huyo akibanjuka na njemba.
Wawili hao, baada ya kubambwa 'laivu' walitiwa kizuizini kabla ya
vijana wanaodaiwa kuchukua posho kwa wanaofanyia mambo yao kwenye
danguro hilo kuanzisha vurumai ingawa walidhibitiwa huku jamaa aliyekuwa
anahudumiwa akitoka nduki.
Akizungumza na gazeti hili, mwanamke huyo aliomba asamehewe na kusema
kwamba kinachomsababishia kufanya shughuli hiyo ni ugumu wa maisha na
kundi la watoto anaowalea ambao baba yao hana ajira.
Gazeti hili lilipotaka kuzungumza na mumewe ili kujua kama anafahamu
kuwa mkewe anafanya biashara haramu ya kuuza mwili, mwanamke huyo alidai
kwamba mumewe hana simu.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisikika akisema: "Dah! Mngewahi dakika kumi tu, mngemkuta baba wa Kiarabu aliyeingia na mwanamke muda si mrefu, hili danguro linatumiwa usiku kucha, yaani linapoingia giza tu hapa ni balaa hadi asubuhi."

Mwalimu wa zamu, Kilavo Charles, aliiambia OFM kuwa suala hilo
limeshafikishwa kituo cha Polisi Mabatini ambao waliahidi
kulishughulikia.“Ni aibu, asubuhi watoto wanafagia kondom, tunakosa cha
kuwaambia, hii ni hatari kwa kweli na tunaomba mamlaka zinazohusika
zilifanyie kazi jambo hili,” lisema.
0 comments: