HIZI NDIO FAIDA 5 ZA KUNUNIANA NA LOVE WAKO !
YAWEZEKANA
kuwa ni mada ambayo imekuachahoi mpenzi msomaji wangu huku ukijiuliza
kama ni kweli zipo faida kwa watu wanaopendana kwa dhati kununiana.
Faida
ipi hiyo zaidi ya maumivu na mateso ya moyo? Jamani ni kweli kabisa
kwamba kuna maumivu na karaha nyingi unaponuniana na mpenzi wako, lakini
wakati huo huo kuna faida nyingi za kununiana naye. Mapenzi yana wigo
mpana mno ambao mtu anapaswa kuuangalia kwa jicho pana na akili pembuzi
kabla ya kuingia,namaanisha kwamba ni lazima kuchunguza kina cha maji
kabla ya kuzamia. Sasa basi, zifuatazo ni faida tano utakazozipata ukiwa
umenuniana na mpenzi wako.
HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO
Ni
ukweli usiopingika kuwa, katika hali ya kawaida, ukiwa mbali na mtu
fulani katika jamii unayoishi ni vigumu sanakujikuta umekwaruzana naye.
Hii ni kwasababu utakuwa hauingiliani nayekatika mizunguko yako, vivyo
hivyo kwa wapenzi walionuniana.Hali hii hupunguza kabisamigogoro ya hapa
na pale, kwani hiki ni kipindi ambacho mtakuwa mbalimbali jambo ambalo
huepusha maudhi ya kibinadamu.Mfano, yawezakana katika kipindi
mlichonuniana na mpenziwako, uliingia ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake
kutoka kwa mtu aliyekosea namba. Kwa kuwa hauko naye karibu jambo hili
halitakuumiza maana hutaelewa nini kimeendelea tofauti na kama
ungelikuwa naye karibu.Kwa hiyo kuna baadhi ya maumivu na maudhi ambayo
utaepukana nayokwa kipindi cha kununiana kwenu. Ni kweli kabisa kwamba
hupunguza migogoro na mitafaruku ya hapa na pale, umeelewa mpenzi
msomaji wangu? Haya twende kwenye faida ya pili.
KUBAINI TABIA X ZA MWENZAKO
Hiki
ni kipindi ambacho sasa kitakusaidia wewe kubaini tabia na mienendo
mibaya ya mwenzi wako. Hii ni kwa kuwa utakuwa mbali naye hivyo naye
hujiona kuwa yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila
kujali uwepo wako kwani kila mtu ana ‘time’ na mwenzake.Kama kuna asili
ya maisha yake ambayo aliiacha baada ya kuingia katika uhusiano na
wewe,ambayo ni mbaya zaidi sasa hapa ataanza kuirudia kwa kujiona kuwa
hana mtu wa kumzuia na kumbana.Kama ni mlevi kupindukia,mchafu, muongo
na tabia nyingine mbaya za kufanana na hizi basi ataanza kuzionesha
katika kipindi ambacho mmenuniana.
KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI
Hapa
naomba nieleweke vizuri kabisa kwamba, ninapoongelea suala la
kutafakari zaidi katika kipindi ambacho wewe hauna maelewano mazurina
mwenzi wako, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa kutafakari
penzi lenu kwa ujumla.Ni kipindi kitachokuongoza wewe kuwa na uelewa wa
ni aina gani ya mpenzi uliyenaye. Kivipi? Ni kwamba, katika muda huu
mara nyingi utataka kupata suluhu ya kununiana kwenu, lakini pia katika
kutafuta suluhuhiyo utapata fursa ya kutafakari kwa kina juu yapenzi
lenu huku ukimpima mwezi wako kwa mtazamo chanya.
KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE
Si
kila rafiki wa mwenza wako ana nia nzuri na uhusiano wenu au anafurahia
penzi lenu. Mathalani, labda wewe ni msichana na pengine miongoni mwa
rafiki zakekuna mmoja au wawili ambao hutamani sana kupata penzi
lako.Sasa katika kipindi ambacho utakuwa umenuniana na mpenzi wako basi
itakuwa ni nafasi nzuri kwao kuitumia kunyunyizia sumu ya kumponda huku
wakikutamkia maneno ya kukushawishi, hivyo utakuwa umeelewa ni aina gani
ya marafiki alionao mwenzi wako.Hii si kwa msichana tu, hata kwa
wanamume kwani huenda kati ya rafiki wa ‘girlfriend’ wako, kuna
wanaokutamani, sasa wakiona huna uhusiano mzuri na mpenzi wako,
watatumia nafasi hii kukuambia maneno ya uongo juu yake na kukuonesha
kila dalili za kukutaka.Hivyo utakuwa umefahamu ni aina gani ya rafiki
ambao mpenzi wako anao. Tambua kwamba, marafiki wengi wana tabia
zinazofanana.
KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO
Katika
kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi alilonalo huyo mtu
wako juu yako. Kwa mpenzi aliye na hisiaza dhati kabisa kwako, katika
kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo
lenu.Pamoja na kwamba wewe utakuwa umenuna, bado yeye ataonesha kukujali
kama kawaida, atakupigia simu za hapa na pale yaani ilimradi tu asikie
angalau sauti yako,lengo lake likiwa ni kutaka kurejesha ukaribu ambao
sasa anaona kama akiupoteza itakuwa ni maumivu kwake.Kwa mantiki hiyo
basi, utagundua ni kwa jinsi gani anathamini penzi lenu na ni aina gani
ya penzi alilonalo kwako. Yote haya utabahatika kuyajua kupitia kipindi
cha kununiana kwenu.Hata hivyo, niwatahadharishe kwamba, kuandika haya
isiwe ni tiketi ya wewe sasa kuanza kununiana na mpenzi wako eti kwa
kigezo kwamba utapata nafasi ya kumfahamu, la hasha! Siku zote katika
uhusianowako epuka maudhi na migogoro isiyokuwa ya maana.
0 comments: