KOFI ANNAN: EBOLA NI UGONJWA WA WATU MASKINI NA SIO MATAJIRI
Mwana
Diplomasia kutoka Ghana ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa
Mataifa (UN) Kofi Annan amesema ugonjwa wa Ebola ni wa ‘maskini’ na sio
matajiri.Annan amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha
CNN ambapo amezungumzia sababu kadhaa zinazopelekea mapambano ya dhidi
ya Ebola kuchukua muda mrefu huku maelfu ya watu wakipoteza
maisha.Katibu Mkuu huyo mstaafu amesema Ebola ni ugonjwa wa maskini kwa
kuwa tangu ugundulike ni takribani miaka 40 imepita, ambapo kwa nchi
tajiri ingewezekana kufanyika tafiti ambazo zingesaidia kupata ufumbuzi
wa tiba ya ugonjwa huo, kitu ambacho nchi maskini za Afrika hazina uwezo
wa kuwekeza kwenye tafiti hizo.
Aidha, Annan ameonekana kuvunjwa moyo na jitihada zinazofanywa na
mataifa makubwa ikiwemo Marekani kutangaza utaratibu mwisho wa wiki
iliyopita wa kuwaweka karantini wauguzi na madaktari waliotoka Afrika
Magharibi kwa siku 21, kitu ambacho kinarudisha nyuma ari ya wahudumu
hao kujitolea kusaidia wagonjwa kwenye nchi zilizoathirika na Ebola.
Amesema njia pekee ya kuimaliza Ebola ni kufanya jitihada na
mapambano ya pamoja katika kuzisaidia nchi za Afrika Magharibi na sio
kwingineko, na kuongeza kuwa Afrika inachohitaji ni msaada wa vifaa,
madawa na wauguzi ili kupambana na Ebola.
Mpaka sasa Liberia, Guinea na Sierra Leone zimetajwa kuathiriwa zaidi
na Ebola,huku takwimu zikionesha zaidi ya watu 4,900 wamefariki na
wngine zaidi ya 10,000 kupatwa na maambukizi ya ugonjwa huo.
0 comments: