USIWE NYUMA JUA HAYAAA..Mapenzi Matamu Sana, Fahamu Njia 18 Za 'Kumshika' Kidume Yeyote Ulimwenguni
Unapokutana na mwanaume
akakutongoza/mwanamke akakukubalia kuna uwezekano mkubwa kuwa amevutiwa na wewe
kweli au kakutamani tu. Kitu ambacho watu hua wanasahau ni kwamba hata mtu
aliyekutamani tu unaweza ukampa mwongozo/sababu mpaka mwenyewe akajikuta
anakupenda kuliko ambavyo angeweza kutarajia kwamba angewahi kupenda.
Ndio maana hata wale waitwao 'bad
girls/boys' hua wanajikuta wamenaswa na kunasika at some point.
1. Usiigize.
Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa
vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/mazoea n.k
2. Don't move too fast/act desperate.
Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa
wa mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo gani na mie?"
"utanioa?" "Kanitambulishe/nataka nikakutambulishe." n.k
Mpe nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa aina gani, je unafanania
na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly hata ndoani? Na
wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho hicho.
3.Don't be too demanding.
Huyo sio baba yako wala sio mume
just yet, hivyo chochote atakachokufanyia kinatokana na yeye kutaka/kupenda
kufanya hivyo na sio kwakulazimika. Haki hiyo hauna.
4. Kuwa na shukurani.
Learn to appreciate all that he does
for you, that way ataona umuhimu wa hayo anayokufanyia, yawe makubwa au
madogo.
5. Be real.
Badala ya kufika kwake na kuanza
kushangaa anaishije bila ya mfanyakazi wa ndani huku ukitamba kuwa wewe huwezi,
shangaa anawezaje weka nyumba yake katika hali nzuri mwenyewe bila ya msaada.
Hii itaonyesha fika wewe utakua mke wa aina gani hapo baadae, kama ni wale
wakukaa miguu juu huku wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au la.
6. Learn to cook if you don't know how to.
Waliosema "the way to a man's
heart is through his stomach" hawakukosea. Ukiachilia mbali wale watu
wachache wanaokula ili kushiba wengi hua wanajali ladha. Hiyo ndio hua
inawaongezea hamu ya kula na kuwarudisha nyumbani mapema pia kuwafanya wakumiss
pale inaposhindikana kula chakula chako . Kwakumwonyesha mwanaume kwamba hata
tumbo lake unaweza kuliridhisha unamwongezea sababu za kukuweka kwenye maisha
yake.
7. Mheshimu.
Mpe heshima yake kama mwanaume wako
ila usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba
haheshimiki.
8. Kuwa ngao yake.
Inapotokea anakumbwa na matatizo
yoyote yale onyesha utayari wa wewe kuwa pamoja naye kwa hali na mali mpaka
yatakapoisha. Pia usikose kumjali kumpa moyo pale unapoona inahitajika.
9. Kuwa muwazi.
Kama kuna mambo ambayo unajua moja
kwa moja yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze
mapema ili aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la.
10. Usiwe na chuki.
Kikifika kipindi cha yeye
kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake onyesha ushirikiano. Usionyeshe chuki
wala kujiona kana kwamba wewe ndio wewe. 11. Give your all. Kama na nyie
mtaamua kuonjeshana tunda kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi
kuwa mbunifu, mtundu na usiwe mvivu.
12.Pendeza.
Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje
hata ndani pia. Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu mavazi yako.
13. Onyesha interest kwa yale ayapendayo yeye.
Usiwe mbinafsi kila siku unataka kusikilizwa wewe tu na story/mambo utakayo wewe. Uliza/jua kuhusu yale anayopenda yeye mf. mpira/siasa.
14.Kuwa mtulivu.
Usiwe mtu ambae kila saa simu yako
inapigwa pigwa na wanaume wasio ndugu wala marafiki wakaribu na wanaoeleweka.
Discpline ni muhimu sana.
15.Usimzonge.
Usiwe mmoja wa wale watu
wanaofuatilia wenzi wao masaa yote wanapokuwa hawapo pamoja. Mpe nafasi ya kuwa
na marafiki zake bila kuhitaji kuzima simu ama ku-ignore simu/text zako.
16. Mfurahishe/chekeshe.
Joke around sio muda wote yeye ndio
awe wakukufurahisha wewe.
17. Jifunze kusamehe.
Mambo madogo madogo yanapoombewa
msamaha samehe na uache yapite.
18. Mshirikishe Mungu wako.
Ukishaona kwamba huyo ndie basi
mshirikishe yule unayemwamini ili upate mwongozo wa kiroho. Naamini kwa mada
hizi, mwaka huu mtanishukuru sana. Ushindwe mwenyewe na Mpenzi wako. Mia Credit
kwa threewhite
0 comments: