USHAURI JAMANI: MKE WA RAFIKI YANGU ANANITAKA KIMAPENZI
Familia yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko tayari kukopa mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume). Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially akina mama.
Hivi karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye, naye yuko mbali na mkewe japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi miwili hivi, then hurudi kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa akinisumbua sana mara kwa mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani nilimpa, akanirudishia. Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa ulipofika akaniambia kuwa Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela, hivyo afanye atakaloweza kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba nimkopeshe tena, basi nikawa mpole tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela kubwa (30,000).
Baada ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake anaumwa anatakiwa aende kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr. atatuma hela wiki ijayo. Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake akafariki ikawa ni msiba huku mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole. Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua alipatwa na matatizo, acha iwe msaada.
Baada ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa anamdai laki 4, ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa nimshauri afanyeje maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba alitaka nimsaidie tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo kidogo hivyo hivyo.
Siku moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna kitu anataka kuniambia. Nilipompigia alinishukuru kwa yote niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo baadaye akaniambia njoo tulale, nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji kuwa na mimi. Ameniambia hawezi kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo na liwe lazima awe na mimi anipe tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata simu na tangu hapo nimejikuta kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na hali ya kuchanganyikiwa kimawazo. ananitumia message za mapenzi kibao, japo mimi nimeamua kutokujibu message hizo.
Najua
fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu ni kuwa haya yote
yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na familia yake.
Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na hatumi hela kwa
visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau, naombeni comment
zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the situation. Sisemi
kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna wakati wa kupata na
kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe mwanaume fanya juu
chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni wako, lakini hawa
wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia majaribuni. Mimi
sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya mapenzi lakini
mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani alaumiwe?
0 comments: