MHE ZITTO KABWE- NAKWENDA KUANZA KAZI RASMI MTWARA 31/12/2014 NITAZUNGUUKA NCHI NZIMA NA PROF LIPUMBA
"Kuweka rekodi sawa, PAP ( sio IPTL ) wamelipwa tshs 306 bilioni. Alizosema Rais ni zile zilizokuwa Benki kama taslimu na dhamana za Serikali.
Ambazo hakusema ni zile ambazo zililipwa na TANESCO baadaye.
Ifahamike hadidu rejea ( Terms of References ) kwa CAG kufanya uchunguzi zilitolewa na PAC, hivyo PAC ndio yenye mamlaka ya kuzisemea, kuzielezea na kuzitolea ufafanuzi.
Kwenye eneo hili Rais hakuwa sahihi na Ikulu inapasa kurekebisha. Jumla ya fedha ambayo PAP wamelipwa kutoka akaunti ya TegetaEscrow Ni tshs 306 bilioni.
Muhimu sana
Mamlaka ya Kutafsiri Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali haipo kwa mkaguliwa ( Serikali ) Bali kwa Bunge. Bunge hufanya kazi hiyo kupitia Kamati ya PAC."
0 comments: