Mkazi wa kijiji cha kibara anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutengeneza noti bandia
Jeshi
la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kibara
wilayani Bunda mkoani Mara Jonathani Daniel (33) kwa tuhuma za
kupatikana na noti bandia 75, za shilingi elfu kumi kila moja zenye
thamani ya shilingi 750,000, pamoja na vifaa vya kutengenezea pesa hizo
bandia.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kamanda wa
Polisi mkoani Shinyanga Bw. Justus Kamugisha amesema tukio hilo
limetokea Desemba 27 mwaka huu,majira ya saa 2:00 usiku katika eneo la
kituo cha basi kwenye kijiji na kata ya Kakola tafara ya Msalala
wilayani Kahama.
Amesema
mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wa jeshi hilo wakati wakiwa katika
doria ya kawaida kwenye kituo hicho cha mabasi akiwa na noti hizo bandia
na kuwa kati yake noti 3 zina namba BL, 0315207, noti (32) BB 0315203, noti (21) BE 0315206 , na noti (19) zikiwa na namba BC 0315209.
Kamanda
Kamugisha ameongeza kuwa licha ya kumkamata mtuhumiwa na noti hizo
bandia, pia amekamatwa akiwa na bando ya karatasi , Sindano pamoja na
chupa ya konyagi iliyokuwa na unga mweupe, vifaa ambavyo vinasadikiwa
kutengenezea noti hizo.
Aidha
kamanda Kamugisha ameongeza kuwa Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa
mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazo mkabili mara baada ya
upelelezi wa jeshi hilo kukamilika.
0 comments: