Ukawa kutumia nguvu ya umma kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na rais kama maadhimio ya bunge hayatatekelezwa kiusahihi
Vyama
vya siasa vinavyounda UKAWA vitatumia nguvu ya umma kuing'oa madarakani
serikali ya chama cha mapinduzi kwa kuwapigia kura ya kutokuwa na imani
waziri mkuu na Rais Kikwete kama leo haitatekeleza maazimio ya bunge ya
kuwawajibisha wote waliohusika na sakata la uchotwaji wa fedha akaunti
ya Tegeta Ewscrow.
Naibu
katibu mkuu wa chadema Mh. John Mnyika amesema hayo katika mkutano wa
hadhara katika manispaa ya moshi kuwapongeza wananchi wa manispaa hiyo
kwa kuonyesha imani na chama hicho na kukipatia ushindi wa mitaa 31
dhidi ya 29 ya CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mh.
Mnyika amesema, kura hizo zitapigwa na wabunge wa ukawa ambao pia
watafanya kazi ya kuwahamasisha wananchi wajiandikishe kwa wingi katika
daftari la wapiga kura ili kuipigia kura ya hapana katiba
inayopendekezwa mwezi aprili mwaka 2015 na kuwawezesha pia kupiga katika
uchaguzi mkuu ujao na kuing'oa CCM.
Mwenyekiti
wa chadema mkoani kilimanjaro Mh.Philemon Ndesamburo amewataka wananchi
wakubali kufanyika mabadiliko katika uchaguzi mkuu ujao ili UKAWA
ambayo imedhamiria kuchukua madaraka ya nchi iweze kuwaletea maendeleo
ya kweli.
0 comments: