ESCROW: KKKT WAMCHARUKIA KIKWETE...WANAOJIHUSISHA NA UFISADI WASIWEKWE VIPORO
Kanisa
la kiinjili la Kilutheri dayosisi ya kaskazini (KKKT) limeitaka
serikali isiache viporo katika kuwachukulia hatua za kisheria watumishi
wa umma wanaojihusisha na vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya
raslimali za taifa kwa manufaa yao kwa kuwa hali hiyo inawakatisha tamaa
watanzania.
Rai
hiyo imetolewa na askofu mteule wa kanisa hilo Dr Fredrick Shoo baada
ya kusimikwa rasmi kushika nafasi hiyo kuchukua nafasi ya askofu Dr
Martin Shao aliyestaafu katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa
serikali na vyama vya siasa akiwemo mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya
IPP Dr Reginald Mengi.
Askofu
Dr Shoo amesema, inasikitisha kuona bado kuna taarifa za kuenea kwa
ufisadi mkubwa miongoni mwa viongozi wa serikali na baadhi yao
wakionyesha ujeuri na ukakamavu huku viporo vikiendelea kukaa muda mrefu
ambavyo mwisho wake kuwa sumu ambayo madhara yake ni makubwa kwa taifa.
Wakizungumza
katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na waziri mkuu mstaafu Mh Edward
Lowasa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe
maaskofu Isaack Amani wa kanisa katoliki na mkuu wa kanisa la KKKT Dr
Alex Malasusa wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani kuelekea katika
matukio makubwa mawili mwaka huu ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu.
Katika
hotuba yake iliyosomwa na waziri wa nchi ya rais utawala bora Mh George
Mkuchika rais Kikwete amesema, serikali itaendelea kushirikiana na
madhehebu ya dini kuboresha huduma za jamii ikiwemo sekta ya elimu
ambayo imeanza kuleta mafanikio hasa katika shule za sekondari za kata.
0 comments: