RONALDO MWANASOKA BORA WA DUNIA 2014


Mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo akiwa na tuzo ya Ballon d'Or baada ya kutangazwa na FIFA kuwa Mwanasoka Bora wa mwaka 2014.
Cristiano Ronaldo (kushoto) akisalimiana na Rais wa UEFA, Michel Platini.
Mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo.
MCHEZAJI wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya FIFA ya Mwanasoka Bora wa mwaka 2014 maarufu kama FIFA BALLON D'OR ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo.
Ronaldo amewashinda Lionel Messi wa Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina pamoja na golikipa wa timu ya taifa ya Ujerumani na Bayern Munich manuel Neuer.
Ronaldo ameshinda kwa kupata 37.66% ya kura zote zilizopigwa, akifuatiwa na Lionel Messi aliyepata 15.76% wakati @Manuel_Neuer akipata 15.72% ya kura zote.
Katika Tuzo hizo, kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Low ametajwa kuwa Kocha bora wa FIFA wa mwaka 2014, na James Rodrigues amepata tuzo ya bao bora la FIFA la mwaka 2014 na kutunukiwa tuzo ya FIFA PUSKAS AWARD kwa bao aliloifungia Colombia katika mchezo wa Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay.

Kikosi bora cha FIFA ni Neuer: Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben.

0 comments:

Copyright © 2013. MAPYATZBLOG - All Rights Reserved
Customized by: MAPYATZBLOG | Powered by: http://bongoswagzs.blogspot.com/
Designed by: http://bongoswagzs.blogspot.com//