WAKE ZA WATU OVYOOO!!.. WAJITOA FAHAMU NA KUMWAGA RADHI
Mtu mzima ovyoo! Akina
mama watatu ambao ni wake za watu, wanaounda Kundi la Heshima Pesa
Shikamoo Makelele lenye maskani yake maeneo ya Mawenzi mjini hapa
wanadaiwa kuwachefua baadhi ya watu baada ya kujitoa fahamu na kumwaga
‘lazi’ hadharani na mbaya zaidi mbele ya watoto wadogo.Kwa
mujibu wa ‘shujaa’ wetu, tukio hilo la aibu ya aina yake lilijiri
juzikati kwenye Ukumbi wa Savoy mjini hapa ambapo wanawake hao
walialikwa kuburudisha kwenye sherehe ya harusi ya jirani yao.
Wanawake
hao waliofahamika kwa majina ya watoto wao ni pamoja na mama Sabra
aliyekuwa akibinuka, aliyevalia kigauni kifupi cha draftidrafti.Mwingine
alikuwa ni mama Jenifa aliyekuwa ametupia kimini cha njano na mama
Athuman ambao kwa pamoja walikuwa na vikuku miguuni.
Mtu
wetu huyo aliyekuwa ndani ya ukumbi huo aliwashuhudia wanawake hao
wakimwaga lazi mara baada ya MC kuita kundi lao kwa ajili ya kutoa
zawadi.
Kabla
ya kutoa zawadi, wamama hao walimfuata DJ na kumtaka kuwawekea wimbo
wowote wa Taarab, wakawekewa ambapo wakiwa na zawadi yao ya doti moja ya
khanga, walipita mbele ya maharusi kwa mbwembwe zote na baada ya
kukabidhi zawadi hiyo ndipo balaa lilipoanza.
Huku
wakipeana nafasi na mara nyingine kulaliana, walikuwa wakijibinua na
kuonesha staili za chumbani huku ‘makufuli’ yakiwa nje, jambo
lililotibua harusi hiyo.
Ilifika
hatua hadi baadhi ya wazazi wakawa wanawaziba watoto wasione, jambo
lililosababisha wazazi wa pande zote mbili (wakwe) kununa pamoja na MC
wa shughuli hiyo, MC Chuma ambaye baada ya kuona wanawake hao wanazidi
kuvua nguo aliwashtua:
Wakwe wakichoshwa na tabia chafu za wanawake hao.
“Ninyi
mnaofanya hivyo mjue OFM (Oparesheni Fichua Maovu ya Global Publishers)
ipo humu ndani, sasa kesho au keshokutwa msitafute lawama.”
Pamoja na angalizo hilo la MC, ndiyo kwanza wanawake hao walipozidi kumwaga lazi ikawa ni laana tupu.
Baada ya pati kukamilika, mwanahabari wetu aliwafuata wanawake hao na kuwahoji kulikoni kumwaga radhi kiasi hicho? Msikie huyu:
Huyu ni Mama Sabra aliyekuwa alimwaga radhi waziwazi.
“Kazi
yetu ni kuchangamsha sherehe. Shughuli ilipooza lakini baada ya sisi
kuserebuka, ilibadilika, habari ndiyo hiyo,” alisema mama Sabra.
0 comments: