NOMA SANA OFM YAMNASA HAUSIGELI AKIJIUZA , MWENYEWE AJITETEA KUWA NI UGUMU WA MAISHA
Tumekwisha!
Kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers,
kimemnasa msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli) akifanya biashara haramu
ya kuuza mwili kwa kisingizio cha mshahara kiduchu.
Kushoto ni hausigeli akifanya biashara ya uchangudoa maeneo ya Sinza jijini Dar.Mara baada ya kumnasa na kumlamba picha akiwa na wenzake ambao nao kama yeye walikuwa wamevaa nguo fupi yaani nusu utupu, alianza kuangua kilio hasa alipokuwa akihojiwa kwa nini anajihusisha na biashara hiyo hatarishi katika maisha yake.
“Jamani mmenipiga picha mtanipotezea kazi yangu, jamani mimi nimeajiriwa, ni mfanyakazi wa ndani kwa mheshimiwa Mikocheni (Dar), nafanya kazi za ndani hii yote ni kujitafutia riziki nje ya kazi,” alilalama binti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 23.
Binti huyo aliwaambia OFM kwamba alifikia hatua hiyo ya kujiingiza katika biashara hiyo ya ngono kutokana na ugumu wa maisha huku lawama akizielekeza kwenye mshahara kidogo wa kazi za ndani.
“Mshahara wangu ni mdogo sana, nalipwa shilingi elfu 50 kwa mwezi, nina watoto wawili kijijini hivyo hautoshi. Kama vipi nitafutieni kazi nitaacha kuuza mwili,” alisema.
Alipoulizwa namna anavyotoka kwa bosi wake kwenda kujiuza, hausigeli huyo alisema kwamba huwa anakula dili na walinzi wa bosi wake usiku wakiwa wamelala anatoka na akirudi freshi anawakatia walinzi chao.
Machangudoa wengine wakizikimbia kamera za Global.Aliendelea kueleza kwamba kuna siku nyingine huwa anarudi nyumbani akiwa amevuna fedha nyingi kuliko mshahara wake.
“Hii kazi yangu inaniingizia kipato kikubwa sana kuliko mshahara,” alisema hausigeli huyo
0 comments: