NOOOMA SANAAA......MGOMBEA 2015 ANASWA NA DENTI GESTI
HILI
nalo janga! Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia
anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo Kinondoni jijini Dar es
Salaam, aliyetajwa kwa jina moja la mzee Beno amenaswa akiwa chumba cha
gesti na denti wa chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar, Ijumaa
‘kubwa’ lina mkanda wote.
Mwanaume mmoja anayesemekana ni
mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo
Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mzee Beno akificha sura kwa aibu ili
asipigwe picha baada ya kufumaniwa.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20,
mwaka huu ndani ya gesti moja (jina tunalo) iliyopo Kimara-Suka jijini
Dar es Salaam ambako mama mzazi wa wa binti huyo ndiye aliyemnasa
mheshimiwa mtarajiwa huyo na binti yake.WASIWASI KWANZA
Awali, mama huyo alisema alianza kuwa na
wasiwasi na mwenendo wa binti yake huyo kutokana na kuanza kale katabia
ka’ kuchelewa mara kwa mara kurudi nyumbani akitoka chuoni, akajiongeza!
“Sisi tulishajua binti yetu ameanza katabia
kabaya, akienda shuleni anachelewa kurudi wakati si kawaida yake,
tukasema kuna jambo linaendelea kwake,” alisema mzazi huyo
Akidhibitiwa baad ya kufumaniwa.


0 comments: