INASIKITISHA SANAAA..Mume auawa kwa kisu na hawara wa mkewe
Mkazi wa Tarafa ya Mang’ula wilayani
Kilombero, Amon Nyenja amefariki dunia baada ya kuchomwa kwa kisu na
anayedhaniwa kuwa ni hawara wa mke wake mdogo.
Tukio hili lilitokea usikuwa Desemba 23
huko Mang’ula na inadaiwa kuwa marehemu alirudi nyumbani saa 3.30 usiku
na kumkosa mkewe hivyo kuamua kumtafuta katika maeneo mbalimbali.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mang’ula,
Shabani Lichaula na Mkuu wa kituo cha Polisi Mang’ula, Nkilijia Lazaro
walisema polisi inamshikilia mke huyo mdogo wa marehemu huku likimtafuta
mtuhumiwa.
Lichaula alidai kuwa marehemu katika
kumtafuta mkewe huyo alimkuta akiwa amesimama mahali na mwanamume na
mwanamke huyo alikimbia na kutokomea na marehemu Nyenja aliamua kumvaa
mgoni wake lakini alizidiwa baada ya mtu huyo kumchoma kisu cha ubavuni
hadi utumbo kutoka nje.
Lichaula alisema baada ya Nyenja
kuchomwa kisu alipiga kelele za kuomba msaada na wasamaria wema
walijitokeza na kumpeleka Kituo cha Afya Mang’ula.
Mganga Mkuu wa Mang’ula, Eugen Shirima
alisema baada ya huduma ya kwanza walimpatia rufaa ya kwenda Hospitali
ya Mtakatifu Francis, Ifakara kwa matibabu lakini alifariki dunia wakiwa
njiani.
0 comments: