MAKOMANDO WAWAOKOA MATEKA SYDNEY, WAMUUA MTEKAJI

Huyu ndiye mtekaji raia wa Iran, Haron Monis.
WATU
watatu wameuawa akiwemo mtekaji raia wa Iran, Haron Monis aliyekuwa
ameteka watu kwa zaidi ya saa 16 katika mgahawa mmoja jijini Sydney
nchini Australia jana baada ya Makomando kuvamia eneo hilo. Watu wanne
akiwemo polisi wamejeruhiwa wakati wa zoezi la uokoaji.

Mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza.
Mtekaji
huyo alikuwa ameachiwa kwa dhamana kwa makosa mbalimbali aliyokuwa
ameshitakiwa nayo. Moja ya makosa yake ilikuwa kuwatumia barua ya matusi
wazazi wa wanajeshi wa Australia waliofariki wakiwa wanalitumikia jeshi
la taifa hilo nchini Iraq.
Waziri
Mkuu wa Australia, Tony Abbott alisema lilikuwa jambo la kushtua sana
kwamba wananchi wasio na hatia kutekwa nyara na mtu ambaye alikuwa
anashinikizwa kisiasa.
Makomando walifyatua risasi na kisha kuingia ndani ya mgahawa huo huku wakirusha magurunedi.
0 comments: