WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUTOROKA NA ALBINO MKOANI MWANZA
Jeshi la
Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu wanne akiwemo baba mzazi wa
mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Albinism aliyetekwa nyara na watu
wasiojulikana usiku wakiwa wamelala na kuondoka naye kusikojulikana hali
iliyozua hofu kubwa kwa jamii.
Amebainisha
hayo kamishina msaidizi mwandamizi ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa
Mwanza Bw.Valentino Mulowola wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake amemtaja mtoto wa kike aliyetekwa nyara mwenye umri wa
miaka minne Pendo Emmanuel mkazi wa kijiji cha Ndambi kata ya fukalo
tarafa ya mwamashimba wilayani kwimba ambaye ni mlemavu wa ngozi amesema
kuwa tarehe 27 Desemba mwaka huu majira ya saa nne na dakika 30 za
usiku watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Bw.Emmanuel Shilinde kwa
kupiga jiwe mlango na kuvamia kisha wakamchukua mtoto mmoja kati ya
watoto watatu waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo kisha wakatoweka naye
kusiko julikana.
Kufuatia
hali hiyo makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania imetuma timu ya askali
upelelezi watakao shirikiana na askari polisi mkoa wa Mwanza kuwasaka
wahalifu walio husika kumteka nyara mtoto na kutoweka naye
pasipojulikana pamoja na kutoa ahadi ya zawadi ya fedha kiasi cha
shilingi milioni tatu kwa yeyote atakaye fanikisha kukamatwa kwa
wahalifu hao ambapo kikosi hicho kwa pamoja kimewatia mbaloni wahamiaji
haramu saba raia wa Ethiopia na watanzania wawili wanashikiliwa kwa
tuhuma za kusaidia wahamiaji haramu hao kuingia nchini kinyume cha
sheria za nchi.
0 comments: