BABY MADAHA AFUNGUKA YA MOYONII KUWA ANATAMANI KUWA NA MTOTO


Mkali wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha.
Stori: MAYASA MARIWATA
MAHABAT! MKALI wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amesema anatamani kuwa na mtoto lakini bado hajamuona mwanaume wa kuzaa naye na kuanika vigezo vya mwanaume anayestahili kuwa baba bora kwake.
Akibonga mawili matatu na paparazi wetu, Baby alisema suala hilo linahitaji umakini mkubwa katika uchaguzi na sifa anazozihitaji yeye ni upendo wa kweli na uhodari wa chumbani katika uwanja wa mahaba.
“Namsaka mwanaume mwenye sifa za kunizalisha, awe  baba bora maana ishu ya kumpata mwanaume huyo si suala la mchezo lazima uwe makini ili mtoto wako ajivunie kwa mzazi aliyenaye, sichagui rangi ila awe mrefu na mwili uliojijenga, akiwa amenizidi umri au mdogo
freshi tu ilimradi aweze kazi,” alisema Baby.

0 comments:

Copyright © 2013. MAPYATZBLOG - All Rights Reserved
Customized by: MAPYATZBLOG | Powered by: http://bongoswagzs.blogspot.com/
Designed by: http://bongoswagzs.blogspot.com//