RAY C AWAPA SOMO LA UNGA KIBA, DIAMOND
SOMO! Mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ametoa tahadhari kwa wasanii kutotumia madawa ya kulevya (unga) ndani ya mwaka huu 2015 huku akiwatupia jicho zaidi nyota wanaofanya vizuri kwenye gemu kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Ray C ambaye ni mmoja wa wasanii waliotumia madawa hayo na kumpa
mateso makubwa kisha kuamua kuyaacha, amesema anahitaji kuona wasanii
hao wakiwa mstari wa mbele kupiga vita matumizi ya unga na si wao kuwa
wa kwanza kutumia kwani vishawishi huwa vinaibuka zaidi pale msanii
anapokuwa juu kimuziki.
Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba.
“Madawa ya kulevya yanatakiwa kupigwa vita sana na kila msanii,
wasanii wakubwa kama Diamond na Ali Kiba sitapenda kuwaona wakizama
kwenye matumizi hayo mabaya, nahitaji kuwaona wakiwa katika nafasi za
juu, wajihadhari maana umaarufu ndiyo unaoibua haya yote,” alisema Ray
C.
0 comments: