ROSE NDAUKA AKATAA KUMSAMEHE MZAZI MWENZAKE
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Na Laurent Samatta/Amani
DIVA wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa ya rohoni kwamba hatokaa amsamehe mzazi mwenziye, Malick Bandawe.
Akizungumza na Amani, Ndauka alisema alishawahi kufuatwa na mzazi
mwenzake huyo kwa lengo la kumuomba msamaha ili waendelee na mapenzi yao
lakini hakuwa tayari kumsamehe.
“Kuachana tumeshaachana,
kama kurudi huwa inatokea lakini kwangu sipo tayari tena kumsamehe,
anaweza kutokea mtu mwingine wa kunipenda ingawa kwa sasa nahitaji
kupumzika kwanza,” alisema Rose.
Rose na mzazi mwenzake waliachana mwaka jana huku wakificha sababu za kuachana kwao.
0 comments: