WEMA SEPETU AMUA KUJIPUMZISHA KWA BOB JUNIOR..WATUMIA DAKIKA 10 KUONYESHANA UFUNDI KWENYE KONA
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa mapajani mwa Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior'. |
TUJIUNGE TEGETA, DAR
Ishu hiyo iliyopigwa chabo na paparazi wetu hivi karibuni lilijiri ndani ya Ukumbi wa Club 71 uliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo Wema siku hiyo alimtambulisha msanii wake mpya anayesimamiwa na kampuni yake ya Endless Fame anayeitwa Ally Luna.
WAKUTANA
Katika tukio hilo, Wema ndiye aliyeanza kufika ukumbini humo akifuatana na timu yake, akiwemo Petit Man (kama kawa).
Muda mfupi baadaye, Bob Junior naye alifika ambapo alipokutana na Wema walianza kupeana mahaba huku wakigandana kwa zaidi ya dakika kumi.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akizidi kupozi kimahaba na ‘Bob Junior'.
Mbali na Bob Junior, Wema alialika wasanii kibao kwa ajili ya
kumsapoti ambao hata wao walipigwa butwaa baada ya kushuhudia tukio
hilo.Wakiwa katika chumba cha VIP, Wema aliendelea kuwa ‘veri klozi’ na Bob Junior hivyo kusababisha minong’ono ya hapa na pale.
MAPOZI
Katika tukio hilo, kilichowashangaza mashuhuda zaidi ni kitendo cha Wema kukaa mapajani kwa Mbongo Fleva huyo bila kujalia macho ya watu.
Wema Sepetu na ‘Bob Junior' wakiteta jambo.
SALAMU KWA DIAMOND NA ZARI?Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walikwenda mbali zaidi na kuanza kuhisi tabia hiyo ya Wema na Bob Junior ni salamu kwa aliyekuwa mwandani wake na kumwagana Nasibu Abdul ‘Diamond’ na ‘bebi’ wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Hapa naona kama sielewielewi maana ni mara ya kwanza kumwona Wema na Bob Junior wakigandana kiasi hiki tangu walipopelekana mahakamani kipindi kile na ukizingatia Sharobaro (Bob Junior) alikuwa hasimu wa Diamond aliyekuwa mpenzi wa Wema kipindi hicho,” alisema mmoja wa mastaa wakubwa (jina linahifadhiwa). Akaongeza:
Wema Sepetu akimchumu ‘Bob Junior.
“Nakuhakikishia hizi ni salamu kwa Diamond na yule Zari wake. Hapa Wema anajua kabisa salamu zitawafikia.”Baadhi ya mastaa hao walionekana kulaani tukio hilo na kujaribu kumtahadharisha Wema juu ya ukaribu huo kwani kama Diamond atagundua atajua ni ishu za kulipizana visasi.
“Kwa vyovyote Diamond akigundua jambo hili litamfanya ukaribu wake na Wema kuzidi kuwa mgumu na kuurejesha ni ndoto kama wana mpango wa kurudiana.”
WENYEWE WANASEMAJE?
Paparazi wetu alipojaribu kuwadodosa wawili hao juu ya uhusiano wao, kila mmoja aliishia kucheka tu bila kutoa majibu ya kueleweka.
DAKTARI AMUONYA WEMA
Wakati huohuo, mmoja wa madaktari wa mastaa Bongo (jina lipo) amemuonya Wema kuhusu masuala ya mapenzi kwamba, kama ni kweli ameanzisha uhusiano mwingine si vizuri kwani bado akili yake haijatulia tangu amwagane na Diamond hivyo anahitaji muda ili kutuliza akili.
“Wema hatakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa haraka, wala si vizuri kulipiza kisasi kwani anaweza kujikuta pabaya zaidi, haya mambo ya mapenzi yanatesa sana mastaa wengi na nimekuwa nikiwapa huduma za kisaikolojia,” alisema dokta huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011, Mahakama ya Mwanzo Kinondoni jijini Dar ilimhukumu Wema kwenda jela miezi sita au faini ya shilingi elfu 40 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana matusi ya nguoni Bob Junior ambapo alilipa faini na kuachiwa huru jambo lililoibua uhasama mkubwa kati yao.
Hivyo, tukio la kuonekana pamoja na kugandana kimahaba ni ishara njema kuwa sasa wapo vizuri na ule uhasama haupo tena!!
0 comments: