WOLPER ATIBUA UCHUMBA WA NAY

Mwigizaji wa filamu Bongo Jacqueline Wolper.


KIMENUKA! Mwigizaji Jacqueline Wolper ameibua tafrani la aina yake kwa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kumtumia meseji iliyomtia shaka mpenzi wa staa huyo, Siwema.

Tukio hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Nay wa Mitego, Kimara- Korogwe jijini Dar  ambapo ilisemekana Wolper alituma SMS iliyokuwa ikiuliza muafaka wa jambo fulani ndipo Siwema akaja juu na kuanza kumcharukia bebi wake huyo.
Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mpenzi wake Siwema.

Alipoulizwa Nay wa Mitego kuhusiana na ugomvi huo, alifunguka:
“Wolper ni rafiki yangu kitambo, ni mtu wangu tunayeelewana kupita maelezo, hivyo juzikati nilikuwa nikichati naye juu ya kutaka kumshirikisha kwenye video ya wimbo wangu mpya wa Akadumba, Siwema dizaini kama alimaindi kuona nawasiliana naye lakini nilimuelewesha na kila kitu kipo sawa.”

0 comments:

Copyright © 2013. MAPYATZBLOG - All Rights Reserved
Customized by: MAPYATZBLOG | Powered by: http://bongoswagzs.blogspot.com/
Designed by: http://bongoswagzs.blogspot.com//