CHUCHU HANS AFUNGUKIA KUACHANA NA RAY
Staa wa Filamu Bongo, Chuchu Hans akiwa na mpenzi wake 'Ray''.
STAA wa
Filamu Bongo, Chuchu Hans juzikati alifungukia madai ya kwamba
ameachana na mchumba wake Vicent Kigosi ‘Ray’, akaeleza kuwa, hakuna
ukweli wowote juu ya hilo.Chuchu alifikia uamuzi wa kufafanua juu ya
madai hayo juzi kufuatia tetesi zilizokuwa zimeenea kwamba yeye na
kipenzi chake huyo wametibuana na sasa kila mtu kimpango wake.
Akifungukia
juu ya uvumi huo Chuchu alisema: “Kutakuwa na watu wanaosambaza uongo
huo, huwezi kuamini muda si mrefu nilikuwa na baby wangu Ray, tukawa
tunashangaa tu juu ya umbeya huo.
“Nahisi
watu wamechukulia kwamba tumeachana baada ya mimi kuamua kubadilisha
jina nililokuwa nikilitumia kwenye akaunti yangu ya kwanza ya Instagram,
nimetoa neno The Greatest na kubakiza jina langu, ilikuwa ni uamuzi tu.
“Siwezi
kuachana na Ray na hata kama ikitokea tumeachana naamini kabisa Ray
hawezi kurudiana na Johari wala Mainda, hao wanaosema eti kaniacha mimi
karudiana na Johari wanachemka,” alisema Chuchu.
0 comments: