TAARIFA ZA MWANZO KUHUSU NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAPOTEA IKIWA NA WATU 162 LEO ASUBUHI
Ndege ya
AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda
Singapore imepoteza mawasiliano leo asubuhi.Ndugu, jamaa na marafiki wa
abiria waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia QZ8501 wakiwa na majonzi wakati
wakisubiri taarifa kuhusu ndugu zao katika Uwanja wa Ndege wa Surabaya,
Indonesia.
Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi
wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1
kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani
aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014
kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta
0 comments: