NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu
alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye
Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo,
jimboni humo (Picha na Bashir Nkoromo)
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu
alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye
Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo,
jimboni humo
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu
alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye
Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo,
jimboni humo
Mwimbaji wa muziki wa Injili, Frola Nkone akiimba kutumbuiza wakati wa mkutano huo
Mwanamuziki wa muizki wa Injili, Rose Mhando akiimba kutumbuiza wananchi katika mkutano huo wa Nyalandu
Steve
Nyerere ambaye ni Msanii na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM,
akizungumza kabla ya kumwaga vimbwanga vyake vya kuingiza sauti za
viongozi mbalimbali wakati wa mkutano huo wa Nyalandu.
KABLA YA MKUTANO
Nyalandu
na Mkewe Faraja Kota wakiingia kwenye Kanisa la KKKT Usharika wa
Ilongelo kwa ajili ya ibada maalum. Pamona nao ni watoto wao Sera na
Christopher kabla ya kwenda Uwanjani kutangaza azma yake ya kuwania
Urais 2015
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu
akitoa neno la shukrani baada ya ibada maalum katika katisa la KKKT
Usharika wa Ilongelo jimboni humo leo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu
akizungumza na viongozi wa shule ya Kiislam ambayo huhudumia watoto wa
dini zote katika kata ya Ilongelo, shule hiyo ina watoto 74.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akisalimia waumini kwenye Kanisa
la FPCT katika jimbo la Ilongelo alipofika kwa ajili ya ibada maalum
Nyalandu na Mkewe wakitoka katika Kanisa la FPCT baada ya kuhudhuria ibada maalum leo asubuhi. Na Bashir Nkoromo, Singida
Mbunge wa
Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo
baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati
za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari
kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais,
lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa
moto na endapo zitayeyuka hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza
uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida
Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua
mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.
"Kazi zangu nilizofanya
zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka
urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema
Nyalandu
Itakapofika siku ya siku,
nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine
wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya
kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.
Mkutano huo wa jimbo ambao
ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina
Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza
Nyalandu.
HABARI KATIKA PICHA, NYALANDU AKITANGAZA KUWANIA URAIS LEO.
0 comments: