SKENDO! MAMA AJIFUNGUA, MANESI WADAIWA KUMTUMBUKIZA MTOTO KWENYE NDOO
Tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo mkoani hapa lilijiri hivi karibuni ambapo mwanamke aitwaye Zainabu lsmali, mkazi wa Kididimo jirani na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine ‘SUA’ alishikwa na uchungu wa kujifungua na kukimbizwa katika hospitali hiyo kwa msaada wa jirani yake aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sira Manga.
Ndoo iliyotumika.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda juu ya tukio hilo, Mama Manga alikuwa
na haya ya kusema: “Huu ni uzembe mkubwa wa manesi. Tulipofika hospitali
mtoto alizaliwa akiwa hai lakini alikuwa njiti kwani alikaa tumboni kwa
mama yake miezi 7 badala ya 9.
Ndugu wa mama akiwa na mtoto huyo.
“Cha ajabu usiku huo manesi baada ya kumcheki mtoto walisema ni wa
kike lakini eti walidai amekufa hivyo waliamua kuchukua matambara ya
mzazi yaliyotumika kujifungua na kumzoa mtoto huyo na kumuweka kwenye
ndoo ambayo kwa kawaida sisi wazazi huwa tunakwenda nazo leba.“Walituambia tukazike, unajua kutoka hospitali hadi Kididimo juu ya Milima ya Uluguru ni mbali na gari lilichelewa kutufuata hivyo mtoto huyo alikaa kwenye ndoo zaidi ya saa 3.
Mama wa mtoto huyo, Zainabu lsmali
“Tulipofika nyumbani na kumtoa mtoto kwenye ndoo tukamuona anahema na
kufumbua macho baada ya kumtingisha akakohoa ndipo tukamkimbiza tena
hospitali.Pamoja na jitihada za manesi hao, kesho yake mtoto huyo alifariki dunia baada ya kitovu chake kuingiza hewa kwani kilikuwa bado hakijakatwa.
Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo.
Mama wa mtoto huyo, Zainabu alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema: “Roho inauma sana lakini mzungumzaji wa tukio hilo ni mume wangu.”
Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo alipohojiwa na mwandishi wetu alisema: “Ni kweli nimempoteza mwanangu lakini nisingependa kutoa lawama kwa manesi kwani mke wangu bado anaendelea kuzaa.”
Mwandishi wetu alifika hospitalini hapo na kuzungumza na daktari mfawidhi, Dokta Rita Lyamuya ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dokta Rita Lyamuya.
“Ni kweli tukio hilo limetokea kwenye wodi yetu ya wazazi.“Manesi walitimiza jukumu lao la kumhudumia mzazi lakini kwa bahati mbaya tuna changamoto ya umeme kukatika bila taarifa hivyo wakati manesi wakimzalisha alijifungua mtoto njiti.
“Ghafla umeme ulikatika na kutokana na giza, manesi walijua mtoto amekufa hivyo waliwaeleza wanandugu kwamba mtoto amefariki dunia.
“Ndugu walimchukua walipofika kwao na kukitoa kwenye ndoo walibaini mtoto bado yupo hai.
“Walimleta tena hapa hospitali na tulifanya juhudi za kumtibu lakini kwa bahati mbaya amefariki dunia.”
0 comments: