HUYU NDIYE ALIYEMPA ZARI JEURI YA FEDHA
Kibosile Ivan Ssemwanga akiwa na ‘Zari’.
Wengi
wanamjua Zari kutokana na urembo wa kipekee aliojaliwa na mkwanja wa
kufa mtu, akiwa anamiliki ndinga za bei mbaya zikiwemo Ranger Rover
Sports 2014, BMW, Black Chrysler, Audi Q7, Silver Crysler 2008, Mercedes
Benz Convertible na nyingine kibao, zote zikiwa na ‘plate number’
inayosomeka jina lake la Zari.
Hata
hivyo, ni wachache wanaojua siri ya utajiri wa mwanadada huyo ambaye
kiasili baba yake ana mchanganyiko wa Burundi na Somalia wakati mama
yake ana mchanganyiko wa Mhindi na Mganda.
IVAN SSEMWANGA NDIYO KILA KITU
Kabla ya
kuanza ‘projekti’ na Diamond, Zari alikuwa ameolewa na mfanyabiashara
mkubwa wa Kiganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Ivan
Ssemwanga ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea wachache kutoka
Uganda, akiwa anaingiza faida ya zaidi ya shilingi za Uganda milioni 700
kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 428 za Kibongo).
MALI ANAZOMILIKI IVAN
Achana na
magari ya kifahari ambayo hayana idadi, yote yakiwa na ‘plate number’
yenye jina la Ivan, mchizi pia anamiliki Private Jet (ndege binafsi).
Pia anamiliki utitiri wa vyuo vya Brooklyn City College, vikiwa na jumla
ya ‘campus’ sita nchini Afrika Kusini katika Majiji ya Durban, Pretoria
na Johannesburg, kila moja ikiwa na wanachuo kati ya 800 hadi 2100.
Watoto wa Zarinah Hassan, ‘Zari’.
Kozi
zinazofundishwa kwenye vyuo vyake ni Information Technology (IT), Mining
(uchimbaji wa madini) na Policing (Sera za biashara) ambazo zinapendwa
na wengi Afrika Kusini, hali inayofanya apate wanachuo kibao.
Pia jamaa
anamiliki bonge moja la mjengo lililopo Sir Apollo Kaggwa Road, Kampala
pamoja na nyumba nyingine za kifahari zilizotapakaa maeneo ya Munyonyo,
Bunga, Mutungo na Mukono nchini Uganda.
Pia jamaa
anamiliki nyumba nyingine iliyopo Waterkloof Glen jijini Pretoria,
Afrika Kusini na kuwa miongoni mwa Waganda wachache wanaomiliki nyumba
nchini humo. Pia ana utitiri wa supermarkets, maduka ya vito vya thamani
na maduka ya nguo (boutique) nchini Afrika Kusini.
KUFURU YA FEDHA
Hivi
karibuni, Timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes ilikuwa na mechi dhidi
ya Timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) ambapo jamaa alifanya kufuru ya
aina yake kwa kutoa shilingi milioni 10 za Uganda (zaidi ya shilingi
milioni 6 za Kibongo) kwa kila mchezaji na kuahidi kutoa shilingi
milioni 5 za Uganda (zaidi ya milioni 3) kwa kila atakayefunga bao.
Zarinah Hassan ‘Zari’, 'The Boss Lady' akipozi.
Kama hiyo
haitoshi, jamaa alikodi helikopta iliyombeba yeye na wapambe wake 10
aliosafiri nao kutoka Afrika Kusini na kuwalipia kila kitu kuelekea
kwenye Mji wa Namboole, Uganda kushuhudia mechi hiyo ambayo hata hivyo
Uganda haikushinda.
AMETOKEA WAPI?
Ivan
aliyezaliwa kwenye familia yenye uwezo wa kawaida, alisafiri kwenda
Afrika Kusini akitokea Uganda mwaka 2002 kwa msaada wa mpwa wake,
Kyeyune aliyekuwa akifanya biashara ya magari ya kifahari Bondeni.
Baada ya
kukaa naye kwa kipindi kifupi, Ivan naye alianza kujishughulisha na
biashara hiyo ambapo alifanikiwa kutusua kinoma. Maisha yake
yakabadilika, akaanza kuwekeza kwenye biashara nyingine nyingi mpaka
akawa bilionea. Vijana wengi wa Afrika Kusini wanamtambua kwa jina la
Shaba Wa Shaba 9 kutokana na uwezo wake wa kifedha.
ANAMPAJE JEURI YA FEDHA?
Rekodi
zinaonesha kwamba kabla Zari hajakutana na bilionea huyo, alikuwa mtu wa
kawaida sana, akijishughulisha na mambo ya urembo na saluni za kike
lakini walipokutana, kupendana kisha kuoana, ndipo mwanadada huyo
alipoanza kushaini kwa kuendesha ndinga kali na hadhi ya maisha yake
ikabadilika.
Pia
inaelezwa kuwa hata baada ya uhusiano wao kwenda mrama, bado Ivan
anaendelea kumhudumia Zari na watoto wake watatu waliozaa pamoja, Pinto,
Didy na Quincy kwa kuwapa mkwanja mrefu mara kwa mara huku mwanamke
huyo akisimamia miradi mingi ya mwanaume huyo ambaye inaelezwa kuwa
licha ya kutengana, hawajapeana talaka.
Huyo ndiyo Ivan Ssemwanga, kidume anayempa jeuri ya fedha Zari!
0 comments: