INAUMAAA SANAA HII KUTOKA KWA WASTARA: Sajuki aliondoka na nusu ya akili yangu
Muigizaji wa filamu, Wastara Juma Sajuki amesema pengo la mume wake Sajuki halijazibika.
“02.01.2015 Marehemu mume wangu kipenzi Juma Kilowoko
(sajuki)anatimiza miaka 2 tangu atuache tukiwa na majozi tele moyoni
mwetu,” ameandika Wastara kwenye Facebook.
“Ni ukweli usipoingika ameondoka na nusu ya akili yangu maana sifanyi
chochote bila kumfikilia yeye kwa jinsi alivyokua na mawazo mazuri ya
kujenga namkumbuka na nitamkumbuka siku zote za maisha yangu,nampenda na
nitampenda siku zote.
"Hivyo 02.01.2015 kutakuwa na dua itakayosomwa kwenye kaburi lake
kisutu Dar es salaam kuanzia saa nne asubuhi,na badae kutakuwa na dua
nyumbani tabata pamoja na chakula cha mchana kwa watakaojaliwa naomba
tuungane pamoja kwenye dua hii,asanteni nawapenda wote.”
0 comments: