DUNIA INA MAMBO JAMANI! KIM KARDASHIAN AVUNJA NDOA YA MTU! KISA?!!!
Dunia na vioja vingine 2014, eti unaweza kumuacha mpenzi wako kwa kuwa hafani na staa fulani ambaye wewe unampenda?
Mwanamke mmoja ambaye jinalake ni Rahma, kutoka Cairo, Misri, amedai
talaka kwa mumewe kwa kuwa amekuwa si mwaminifu, amekuwa akimsaliti mara
kwa mara kutokana na kile ambacho mwanamke huyo amekisema eti mumewe
anataka mke wake afanane na Kim Kadarshian au muigizaji Haifa Wehbe.
Mara kadhaa mume wa mwanamke huyo amekuwa akimtaka avae na
kutengeneza nywele zake ili afananena mmoja ya mastaa hao, alikataa,
amesema anatazama mambo mengine ya msingi kuyafanya ikiwemo kumlea mtoto
wake wa mwaka mmoja, hivyo asingeweza na hili la kujitengeneza ili
afanane na mastaa hao ambao yeye aliwaita midoli wa kwenye TV!
Kim Kadarshian
Haifa Wehbe, Mwanamitindo, mwanamuziki na muigizaji kutoka Lebanon.
Kwa kuwa dini ya mwanamke huyo inaongozwa na Sheria ya Shariah ambayo
inaruhusu mwanamke kuachika na mahari iliyotolewa kurudishwa, mwanamke
alifanya maombi ya kudai talaka ili aendelee na maisha yake mengine.
0 comments: