BAADA
ya msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga kutangaza nia ya kutaka
kumposa mwigizaji Jacqueline Wolper, staa huyo ameibuka na kumjibu kuwa
na yeye yupo tayari kama ataweza kutimiza masharti. Mwigizaji
wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper akipozi na Manaiki. Akizungumza na
mwanahabari wetu, Wolper alisema katika mila za Kiafrika, posa
haikataliwi, inatolewa na kisha inajadiliwa kwa hiyo kama Manaiki
kajipanga, apeleke posa ikajadiliwe na wazee wake.
“Nimesikia
habari za Manaiki kutaka kuniposa nikacheka sana kwa sababu yeye kama
yupo tayari apeleke posa itapokelewa kwani siku zote vigezo na masharti
huzingatiwa, afuate utaratibu tu,” alisema Wolper.
0 comments: